Tuesday, April 24, 2012

RANGI ANGAVU NDIZO ZIKO KWENYE CHATI SASA


KUNA mambo muhimu yanayopaswa
kuzingatiwa katika mitindo, rangi ni
miongoni mwa mambo hayo. Uwapo
wa rangi katika suala zima la mitindo
ndio hasa msingi mzima wa tasnia hii
yenye wadau wengi duniani. Kwa mujibu wa wataalamu wa mitindo
duniani, kuna rangi za aina mbili; zile
za kudumu kwa mfano nyeupe na
nyeusi na zile za msimu kwa mfano
kijani ya ‘apple’, ‘hot pink’. Kipindi hiki rangi nyeusi na nyeupe
zimepigwa kikumbo kwani rangi
angavu ndizo zilizopo kwenye chati.
Suruali za jeans za rangi ya pinki, bluu,
njano zinavaliwa sana wakati huu
tofauti na zile za bluu, nyeusi na nyeupe, yote hii ni kwa sababu huu ni
msimu wa ‘rangi rangi’ kwenye
mitindo. Rangi hizi endapo zitavaliwa na mtu
yeyote, zina uwezo mkubwa wa
kuvuta hisia za watu wengi
wanaoangalia vazi lake. Pamoja na
kuvaliwa katika mitoko ya aina tofauti,
rangi hizi zina matokeo mazuri sana katika sherehe za wanawake kwa
mfano ‘kitchen part’, ‘Ladies Party’. Awali ilikuwa ni nadra sana kumuona
mtu kuvaa rangi ya chungwa
ukaichanganya na pinki kali, lakini
sasa unaweza kufanya hivyo.
Wataalamu wanashauri ikiwa
zitatumika katika sherehe ni vizuri kutumia pia katika mapambo
yanayotumiwa katika sherehe husika. Rangi zinazotamba sasa ni kama
zifuatazo: Turquouse ; Hii ni rangi
iliyopauka, ambayo kwa kuangalia
ipo katikati ya bluu na kijani. Rangi hii
inapendeza sana ikiwa itavaliwa sio tu
katika shughuli za mchana bali hata usiku pia. Si hivyo tu, pia ni rangi ya mwaka huu.
Nyekundu: Pamoja na kuwa rangi
nyekundu bado inaonekana bado iko
juu kwa mwaka huu katika mavazi.
Hapa tunapata nyekundu za aina
mbalimbali kama vile zile zilizokolea na zile za kupauka. Chungwa: Hapa tunaweza kupata
rangi kadhaa kama vile ‘orange’ za
kukolea, na hata zile za kupauka.
Rangi hizi pia zimejipatia umaarufu
mkubwa hususan katika sherehe za
harusi, ‘send-off’ na ‘kitchen party’. Zambarau: Pia inajumuisha zambarau
za aina mbalimbali. Uzuri wa rangi hii
ni kwamba inaweza kupambwa kwa
kuitumia yenyewe kwa yenyewe, kwa
mfano unaweza kutumia rangi ya
zambarau iliyokolea ukapamba iliyopauka na ukapendeza. Chocolate: Rangi hii ni huwapendeza
sana watu wanene, kwa mujibu wa
wataalamu wa mitindo rangi za giza
hufanya vizuri zaidi kwa watu wenye
maumbo makubwa kuliko zile za
kupauka. Hivyo ikiwa una umbo kubwa si
vibaya ukaichagua rangi hii. Njano: Hii
ni rangi adimu sana, lakini ni miongoni
mwa rangi zenye mvuto sana ikiwa tu
zitapangiliwa vizuri, si hivyo tu ni rangi
inayoonyesha kujiamini. Unaweza kuipamba na ‘blue iris’, zambarau na
hata nyeusi. Bluu: Hii ilikuwa rangi ya
mwaka 2009. Pamoja na hilo rangi imekuwa ikifanya
vizuri sana katika tasnia ya mitindo.
Unaweza kuvaa bluu ya aina yeyote
na kuonekana upo vizuri. Watu wengi
wamekuwa wakiigopa kuitumia
katika shughuli za send-off. Lakini ni rangi bora sana kuliko watu
wanavyofikiria. Kijani: Kwa upande wa rangi ya kijani
kuna rangi ya kijani kavu , kijani ya
‘apple’ zimekuwa zikifanya vizuri zaidi
kuliko nyingine. Pamoja na
hili ,unachopaswa kufahamu ni
kwamba kijani ni miongoni mwa rangi bora kwa mwaka huu. Pink: Hapa kuna rangi kama ‘Hot pink’,
ambayo ukiipamba na zambarau
utaona maajabu ya rangi hii katika
mitindo. Kijivu: Pamoja na kuwa si
watu wengi wanaoipenda rangi hii,
lakini ipo juu. Pamoja na yote haya, nguo zenye
mchanganyiko wa rangi rangi
zisizokuwa na mpangilio pia zipo
kwenye chati wakati huu.
Imeandaliwa na Maimuna Kubegeya

No comments:

Post a Comment