Monday, September 10, 2012

VIPODOZI VIKALI NI HATARI,TUMIA NJIA ZA ASILI

 Badala ya kutumia vipodozi vikali ambavyo wakati mwimgine huweza kusababisha maradhi kama saratani, ni vyema ukatumia vipodozi asilia ambavyo ni rafiki wa ngozi yako.
Hata hivyo aina yoyote ya ngozi ni nzuri hali mradi isiwe na harara, upele au mabaka. Watu weusi na weupe wasipozifanyia ngozi zao matunzo ni lazima ziharibike na zipoteze mvuto.
Katika makala hii, utapata kujua namna ya kuifanya ngozi yako iwe na weupe wa kipekee kwa kutumia  vitu vya asili ambavyo hupatikana jikoni kwako, tena kwa urahisi.
Haya hapa ni mambo ambayo unaweza kuyafanya ili kuing’arisha ngozi yako hajalishi uwe na ngozi nyeusi au nyeupe.
Siri ya limao.
Limao linaweza kuufanya uso wako ukapata weupe wa  kipekee na kwa wale wenye ngozi nyeusi wakawa waang;avu.
Kata limao nusu. Ile nusu nayo ikate nusu, hivyo utapata robo. Sugua limao katika uso wako na uruhusu juisi yake iingie katika ngozi yako.  Baada ya zoezi hilo acha juisi hiyo ibaki usoni kwa dakika 15. Osha uso wako kwa maji ya moto. Fanya hivyo angalau mara mbili kwa wiki, na utaona mabadiliko.


Siri ya asali na maziwa ya unga
Chukua kikombe, weka maziwa ya unga kijiko kimoja, asali kijiko kimoja na juisi ya limao nusu kijiko. Changanya kasha paka usoni na usugue taratibu. Acha ikae usoni kwa dakika 15 na kasha osha taratibu kwa maji ya vuguvugu. Utayaona matokeo baada ya muda mfupi.
 Siri ya nyanya na unga wa mahindi
Chukua nyanya moja, isage kasha changanya na unga wa mahindi. Jaribu kuufanya mchanganyiko wako mwepesi ili upakike na ukae usoni. Sugua uso wako kwa mchanganyiko huo na uache ukae usoni kwa dakika 20
.
Mchanganyiko wa matunda
Chukua tango, nanasi na papai bichi, visage. Mchangayiko laini utakaopatikana hapo ndiyo  dawa yako. Usugue uso wako taratibu kutoka chini yaani kidevuni kwenda juu. Uache ukae usoni kwa dakika 20 kisha osha kwa maji ya baridi.

No comments:

Post a Comment