Tuesday, October 23, 2012

Kushonea ‘ weaving’

MITINDO ya nywele huchangia kwa kiasi kikubwa katika urembo wa mwanamke na hutoa tafsiri mbalimbali juu yake.
Kuna aina mbalimbali za mitindo  ya nywele  ambayo mara nyingi imekuwa ikihusisha kusuka ama kunyoa.
Kuna aina mbalimbali za misuko na kila mmoja una mvuto wake mhusika.
Ushoneaji wa ‘weaving’ ni miongoni mwa mitindo ambayo inayojizolea umaarufu siku hadi siku. Tofauti na mitindo mingine ya nywele mtindo huu hutumika kwa madhumuni tofauti tofauti na kuleta maana.
Mtindo huu unaweza kutumiwa ofisini, kwanye sherehe na hata nyumbani. Ingawa kuna utofauti mkubwa baina ya mtindo mmoja na mwingine. Zipo nywele ambazo hupendeza zaidi ikiwa zitatumika katika maeno ya ofisini, ambapo mitindo mingine huwa haileti maana kabisa ikiwa itatumika katika eneo hilo.
Kwa mfano weving lenye rangi zilizo tofauti kabisa na nywele kwa mfano nyekundu, nyeupe n.k, ikiwa aina hii itatumiaka kama ilivyo itamfanya mtumiaji aonekane kama kichekesho.
Lakini ikiwa aina hiyo ya weaving itatumiwa na mtu ambaye anakwenda kwenye kumbi za starehe ataonekana ametoka bomba hasa akiweza kushonea kulingana umbo la uso wake.
Aina ya ‘weaving’
Mbali na aina za rangi na muonekano, wataamu wa nywele za bandia wanasema kuna aina mbili za ‘weaving’ ambazo ni ndefu na fupi.
‘Weaving’ fupi
Mara nyingi weaving fupi ndio hasa upendeza kwa wanaokwenda ofisini kwani, zina huwa haziitaji marekebisho yeyote, mara baada ya kushonewa tofauti na zile ndefu.
Si hivyo tu aina hii ya weaving huwapendeza pia watu wenye umri mkubwa na kuwafanya wavutie na waonekane wenye kwenda na wakati.
 


Sifa kuu ya aina hii ya weaving ni kumfanya mtumiaji awe huru katika kuendelea na shughuli zake.
Kwa mujibu wa wataalamu wa mitindo ya nywele, aina hii ya weaving ndio hasa sahihi kwa watu wenye sura pana.
‘Weaving ndefu’
Weaving ndefu hupendeza zaidi katika mitoko ya jioni ama shughuli zisizo za kiofisi. Wakati mwingine huwa na sifa ya kuchukua muda wa mhusika hasa zinavyopeperuka na upepo na kuja usoni na kumfanya atumie muda mwingi kuziweka sawa.
Sifa kuu ya aina hii ya ‘weaving’ ni kumpa mhusika nafasi yakubadisha mitindo tofauti hasa ikiwa kuna uhitaji wa kufanya hivyo.
Si hivyo tu aina hii ya weaving zinaweza kutumiwa katika kuboresha muonekano wa maharusi.
Aina hii ya mtindo ni mahususi kwa wale wenye nyuso nyembamba.
Angalizo
Kwa kuwa ‘weaving’ hutengenezwa kwa kutumia   ‘nylon’ ambayo ikipakwa mafuta na kupigwa na jua hubabuka, unashauriwa kutotumia pink losheni kwa ajili ya kungarisha na badala yake kutumia spray maalum kwa ajili ya kung’arishia.
Matumizi ya pink losheni husababisha weaving kukakachaa hivyo kupoteza mng’ao wake wa asili.
Imeandaliwa na Maimuna Kubegeya
Mitindo: Duka la Darling hair/ Peacock hotel

No comments:

Post a Comment